ENGLAND; CHELSEA itaanza na Manchester City katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu England msimu wa 2024/2025 utakaofanyika Agosti 18 uwanja wa Stanford Bridge.
Katika uwanja wa ‘Gtech Community Stadium’ Brentford watawakaribisha Cryastal Palace siku hiyo hiyo.
Ratiba iliyotolewa leo na Chama cha Soka England (The FA) imeonesha ligi hiyo itaanza Ijumaa Agosti 16 ambapo Man United watakuwa Old Trafford kuvaana na Fulham.
Jumamosi ya Agosti 17 ligi hiyo itaaendelea, Arsenal itakuwa Emirates kuwakaribisha Wolves, Ipswich dhidi ya Liverpool, Everton itakuwa Goodson Park kuikaribisha Brighton, katika uwanja wa St James Park Newcastle United watawakaribisha Southampton.
Siku hiyo hiyo, Nottinham Forest watakuwa nyumbani dhidi ya Bournemouth, katika uwanja wa London Stadium zamani Upton Park, West Ham United watawakaribisha vijana wa Unai Emery timu ya Aston Villa.
Ratiba kamilI:https://www.premierleague.com/news/4040106