Chelsea, Liverpool hakuna mbabe

Bao la mapema la Kai Havertz lilikataliwa baada ya sheria namba 11 ‘offiside’ kufanya kazi yake, katika mchezo ambao Mykhailo Mudryk ameonesha kiwango kizuri ikiwa ni mchezo wake wa kwanza wakati Liverpool ikilazimishwa sare ya bila kufungana dhidi ya Chelsea mchezo wa EPL, uliopigwa Anfield.

Mudryk aliingia kipindi cha pili akitokea benchi na kufanikisha kutengeneza nafasi kadhaa, licha ya kukosa nafasi ya wazi ambapo akiwa katika nafasi ngumu dhidi ya Alisson Becker alipiga mpira nje.

Timu hizo mbili zimefungana pointi katika msimamo wa EPL 29. Kikosi cha Jurgen Klopp mpaka sasa hakijapata ushindi katika michezo mitatu ya mwisho, kilipoteza 3-1 dhidi ya Brentford, kikanyukwa 3-0 dhidi ya Brighton. Potter sasa anafikisha mechi sita ugenini bila ushindi wowote kwenye michuano hiyo.

Advertisement

Liverpool inashika nafasi ya nane ikiwa na pointi 29, wakati Chelsea inashika nafasi ya 10 ikiwa na idadi hiyo ya pointi, Brenford anashika nafasi ya tisa, akiwa na pointi sawa na wawili hao, amemzidi Chelsea mabao.

/* */