Chelsea, Liverpool kazi kwao
CHELSEA imepoteza michezo saba msimu huu, Liverpool wamepoteza michezo sita, vipi watalingana idadi endapo Liverpool watashinda leo, wawili hao wanakutana mchana huu kwenye mchezo wa raundi ya 20 kwa Chelsea na 19 kwa Liverpool.
Kinachovutia zaidi katika mchezo huo, timu zote mbili zinaingia zikiwa na pointi 28, sare nne na michezo ya kushinda minne. Liverpool inashika nafasi ya tisa, Chelsea inashika nafasi ya 10. Mchezo utapigwa saa 9:30 mchana.
Michezo mingine ya EPL, itakayochezwa leo Bournemouth itakuwa Uwanja wa Vitality kuvaana na Forest, Uwanja wa King Power, Leicester City watawakaribisha vijana wa Roberto De Zerbi, timu ya Brighton Hove Albion.
Katika Dimba la Saint Mary, Soton itakuwa wenyeji wa vijana wa Unai Emery, timu ya Aston Villa, wakati katika Dimba la London, West Ham itakuwa nyumbani kuwakaribisha vijanawa supa Frankie Lampard timu ya Everton.
Crystal Palace baada ya kuambulia sare dhidi ya Man United, leo watakuwa tena nyumbani Helhurst Park kuwakaribisha Newcastle United.