Chelsea vs Man United mechi ya rekodi

LONDON: Matajiri wa London Chelsea leo watakuwa nyumbani katika Uwanja wa Stamfor Bridge dhidi ya Manchester United kwenye mwendelezo wa Ligi Kuu ya England.
Timu zote mbili bado zinatafuta mwelekeo sahihi kutokana na kudorora makali siku za hivi karibuni, Chelsea wapo nafasi ya 12 wakiwa na alama 40 baada ya michezo 28 huku Manchester United wakiwa nafasi ya 6 na alama 48.
Mara ya mwisho timu hizo zilipokutana , United ilishinda 2-1.

Tangu mwaka 1995 timu hizo zimekutana takribani mara 74, Chelsea wakiibuka na ushindi katika michezo 23 wakati Manchester United wameshinda michezo 22 huku michezo 29 ikimalizika kwa sare.

Mchezo mwingine wa EPL Majogoo wa Anfield Liverpool watakipiga dhidi ya Sheffield United.

Habari Zifananazo

Back to top button