KITENDO cha Arsenal kuhamishia nguvu kwenye usajili wa Moises Caicedo kutoka Brighton, kimewapa nguvu Chelsea kuanza harakati za kumng’oa kiungo huyo wa Ecuador mwenye uwezo pia wakucheza beki wa kulia.
Timu hizo zilikuwa kwenye vita ya kumsajili kiungo huyo tangu mwezi Januari kwenye dirisha dogo la usajili, hakuna aliyefanikiwa, hata hivyo Arsenal waliamua kumchukua Jorginho kutoka Chelsea kama mbadala wa Caicedo.
Imeripotiwa Chelsea kwasasa wameweka nguvu kwa mchezaji huyo licha ya taarifa za Arsenal.
Huenda Chelsea wanasaka mbadala wa Ng’olo Kante ambaye ametimkia Al–Ittihad, huku Mateo Kovacic ikiripotiwa kuwa anatakiwa na Manchester City.