Klabu ya Chelsea imeanza mazungumzo ya kumsaji kiungo mkabaji wa Argentina na Benfica Enzo Fernandez kwa ajili ya kumsajili dirisha dogo la usajili.
Benfica bado hawajathibitisha kupokea ofa yoyote kutoka Chelsea, licha ya timu hiyo kutumia baadhi ya wataalamu wake wa masuala ya usajili kwenda kuangalia uwezekano wa kumnasa mchezaji huyo.
Kwa mujibu wa Fabrizo Romano, Enzo ataanza nje katika mchezo wa leo dhidi ya Braga kutokana na uchovu wa kimwili baada ya mashindano ya Kombe la Dunia.
Amesema Chelsea inajitahidi kusukuma kwa haraka mazungumzo na timu hiyo ili kuinasa saini ya mchezaji huyo.
Chelsea imelazimika kuingia sokoni baada ya baadhi ya nyota wake kuumia katika eneo la kiungo akiwemo Ngolo Kante.