Chelsea yamsajili Badiashile kutoka Monaco

CHELSEA imekamilisha uhamisho wa beki Benoit Badiashile 21, kutoka Monaco ya Ufaransa kwa ada ya uhamisho ya Paundi milioni 35.

Badiashile anadhaniwa kuwa mmoja wa mabeki bora wa kati wanaotumia mguu wa kushoto barani Ulaya na huu umekuwa wasifu wa mchezaji ambaye Chelsea imekuwa ikimtaka tangu majira ya joto.

Advertisement

Badiashile alikamilisha vipimo vyake vya afya Jumatatu na anakuwa ujio mpya wa pili wa Chelsea katika dirisha la uhamisho la Januari. The Blues pia walimfanyia vipimo vya afya kiungo wa kati wa Vasco da Gama Andrey Santos, 18, siku ya Jumamosi.

Tangu Todd Boehly aichukue Chelsea Mei 2022, klabu hiyo imefuata mkakati wa kusajili wachezaji wachanga wenye vipaji.

Wesley Fofana (21), Carney Chukwuemeka (19), Cesare Casadei (19), David Datro Fofana (20) na Gabriel Slonina (18) wote wamesajiliwa na klabu hiyo.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *