Chelsea yathibitisha Cesar kuondoka

CHELSEA imetoa taarifa kuwa nahodha wao, Cesar Azpilicueta amechagua kuondoka klabuni hapo baada ya takribani miaka 11 darajani.

Mwenyekiti wa Chelsea, Toddy Boehly na mmiliki wa Behdad Eghbali wamesema kuondoka kwa Cesar ni heshima kwa klabu hiyo, anaondoka kama mshindi na mchezaji mwenye heshima kubwa.

Mhispania huyo ameripotiwa kuwa huenda akajiunga na Atletico Madrid baada ya kukubali mkataba wa miaka miwili kama mchezaji huru.

Taarifa ya Chelsea pia imempongeza beki huyo ambaye alijiunga na klabu hiyo mwaka 2012 akitokea Marseille ya Ufaransa.

Akiwa Chelsea Cesar amecheza michezo 508, ameshinda mataji tisa, amecheza chini ya makocha tisa tofauti akiwa Stanford.

Habari Zifananazo

Back to top button