Chibu; Sidondoki mpaka Mungu aseme
DAR ES SALAAM: Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva,Naseeb Abdul “Diamond Platnumz” amesema bado yupo sana kwenye muziki mpaka pale Mungu atakapomuambia imetosha.
Amesema hayo Aprili 11,2024 wakati akitangaza ujio wa Tamasha la Muziki litakalofanyika Jijini Dar es salaam Aprili 26,27 na kutamba kuwa mipango yake ni kuendelea kutikisa ndani na nje ya Nchi.
“Suala la kudondoka mimi sidondoki mpaka Mungu aseme, sijui umenielewa? nina ‘hits’ ambazo hazikatiki leo wala kesho mpaka Mwenyezi Mungu akisema Diamond eeh sasa inatosha.
” Lakini kwa maneno ya watu mimi na mawe mimi na nyimbo alafu uzuri Muziki naujua sana” amesema Diamond.