China kuwekeza sekta ya nishati nchini

MFUKO  wa Uwekezaji wa China Africa Development Fund (CADFUND) umeonesha nia ya kuwekeza nchini Tanzania katika sekta ya Nishati kwa kushirikiana na Makampuni ya China na Tanzania.

Taarifa hiyo imetolewa jijini Beijing katika Mkutano wa Waziri wa Nishati January Makamba ambaye yupo ziarani nchini China na Mwenyekiti wa CADFUND,  Song Lei.

Mfuko wa CADFUND wenye mtaji wa Dola za Kimarekani Bilioni 15 ulianzishwa na Serikali ya China kwa madhumuni ya kuwekeza katika miradi uwekezaji barani Afrika ambapo nchini Tanzania mfuko huo umewekeza katika sekta ya kilimo (Uzalishaji wa Mkonge); sekta ya viwanda (uzalishaji wa Saruji) na sekta ya mawasiliano.

Advertisement

Aidha, Kampuni ya China National Offshore Oil Corporation (CNOOC) na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) zimekubaliana kushirikiana katika uwekezaji katika sekta ya gesi nchini ambapo kampuni ya CNOOC imeahidi kuendelea kushirikiana na wadau wengine katika uwekezaji wa ujenzi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta kutoka Uganda hadi Bandari ya Tanga.

2 comments

Comments are closed.