China yahusishwa mchakato sera ya elimu

TANZANIA imeomba msaada wa kiufundi kutoka China ili kusaidia mchakato wa sera ya elimu.

Akimwakilisha Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda, Mkurugenzi wa Elimu ya Juu wa wizara hiyo, Dk Kenneth Hosea ameeleza hayo katika maadhimisho ya kutimiza miaka 10 ya Taasisi ya Kichina ya Confucius iliyopo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Dk Hosea China inaongoza kwenye vipaji pia ina umuhimu mkubwa kwa jamii katika kubadilisha elimu na ujuzi.

Advertisement

Amesema hivi sasa serikali ya Tanzania inaendelea kupitia mitaala ili kuwawezesha Watanzania wawe na ujuzi mbalimbali.

Amesema taasisi hiyo hiyo imekuwa na mchango mkubwa kutoa fursa ya mawasiliano ya kitamaduni na kujifunza lugha ya Kichina kama njia madhubuti ya kuendeleza uhusiano kati ya China na Tanzania.

“Wakurugenzi wa Taasisi za Confucius wanafanya kazi kwa bidii kuhakikisha kuwa vijana wa Tanzania wanajifunza lugha ya Kichina, ili kuboresha uwezo wao wa ushindani katika maendeleo ya kitaaluma na kujiendeleza,” amesema.

Akimwakilisha Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa William Anangisye, Naibu Makamu Mkuu wa UDSM, Bernadeta Killian amesema  chuo hicho kinaanza tena kutoa Shahada ya Kwanza ya Sanaa na Elimu katika  Lugha za Kichina na Kiingereza kwa wanafunzi ambao baadaye watafundisha lugha ya Kichina katika shule za msingi na sekondari nchini Tanzania.

Balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian amesema  hadi sasa taasisi ya Confucius imetoa mafunzo kwa karibu wanafunzi 50,000 wanaojifunza Lugha ya Kichina nchini Tanzania, na kutoa fursa kwa wanafunzi wanaotaka kujifunza lugha hiyo.

Chen amesema taasisi ya Confucius ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, pia imesaidia karibia wanafunzi 100 kutuma maombi ya ufadhili wa masomo na hivyo kuwapa fursa ya kwenda kusoma nchini China.

“Katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, taasisi hiyo imeandaa jumla ya wanafunzi 244 kushiriki katika kambi za majira ya joto za China kwa wanafunzi wa vyuo na sekondari wa Tanzania,” amesema.

 

 

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *