Balozi wa Tanzania nchini China Mbelwa Kairuki ameeleza ameeleza uamuzi wa taifa hilo la Asia kuwa ni: “Habari njema kwa wasafiri wanaokwenda China- kuanzia tarehe 8 Januari 2023 hakuna tena sharti la kukaa karantini siku 8. Wasafiri wanachotakiwa ni kupima uviko19 masaa 48 kabla ya safari. Hatua hii italeta unafuu mkubwa kwa wanafunzi na wafanyabiashara wanaokwenda China.”