China yatoa msaada tetemeko Syria

TAIFA la China limetoa msaada wa dharura wa kibinadamu wenye thamani ya Dola milioni 4.42 kwa Syria, ambao unajumuisha wa Dola milioni 2 na vifaa vya uokoaji vinavyohitajika kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea Februari 6, 2023.

Imeelezwa kuwa China inaharakisha utekelezaji wa mpango wa msaada wa chakula, ambapo tani 220 za ngano na 3,000 za mchele zitatolewa kwenda nchini Syria.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Mao Ning ametoa wito kwa Marekani kusimamisha vikwazo vya upande mmoja dhidi ya Syria ili kushirikiana katika zoezi la uokoaji.

Amesema taifa hilo limekuwa likiingilia mgogoro wa Syria kwa muda mrefu ikiwa ni pamoja na njia ya kijeshi, kuweka vikwazo vikali vya kiuchumi, na kusababisha vifo na majeruhi wengi nchini humo.

Marekani inashikilia maeneo makuu ya uzalishaji wa mafuta nchini Syria zaidi ya 80% ya mafuta yanayozalishwa.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x