Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo ameitakia heri timu ya Yanga katika mchezo wao wa kwanza wa fainali wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaochezwa leo Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu ameitakia heri timu hiyo leo alipokuwa akizungumza katika mkutano na wananchi wa Kata ya Malangali, Jimbo la Mufindi Kusini.
Chongolo yupo Mkoani Iringa kwa ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM, pamoja na kuhimiza uhai wa chama ngazi za mashina, na kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
Comments are closed.