Chongolo ang’aka

Hatuwezi kuwa na nchi kila mtu anaota sharubu!

KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) amekuwa mbongo kutokana na uharibifu wa vyanzo vya maji huku watendaji wa serikali wakishindwa kunusuru hali hiyo.

Akizungumza na wananchi katika Jimbo la Kibakwe wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma, Chongolo amesema atakayebainika kuharibu vyanzo vya maji atachukuliwa hatua za kisheria.

“Mtu akikuambia panda mpaka juu ya mlima hakutaki wewe, haitaki kesho yako. Mkuu wa Wilaya anawajibu wa moja kwa moja wa kusimamia utunzaji wa vyanzo vya maji na kuwa kama kumekuwa na uhalibifu ina maana hajatimiza wajibu wake.

Chongolo ameelekeza wakuu wa wilaya kufanya operesheni maalum kwenye vyanzo vya maji na kuviwekewa alama na kuvilinda na si vinginevyo.

“Tukiacha hivi tutakuwa na Taifa la hovyo huko mbele.., kama mtu hawezi kutii sheria hajue yeye si rafiki wa wengine na hatua za kisheria dhini yake hazitaepukika.”

Pia, amewaonya watendaji wa vijiji kutouza maeneo ambayo yametengwa na kuhifadhiwa kwa ajili ya matumizi maalum.

“Watendaji wote kwenye maeneo yenu mmepewa wajibu, timizeni wajibu wenu, msikae kutengeneza urafiki wa kukusanya sadaka kwenye uhalibifu hilo halikubaliki.

“Hatuwezi kuwa na nchi ambayo kila mtu anaota sharubu na kufanya anachotaka lazima nchi iwe na utaratibu, lazima watu waheshimu sheria na waheshimu maeneo maalum yenye tija tija kwa nchi na si vinginevyo.”

Amesema, matarajio ya CCM kumuona Mkuu wa Wilaya na kamati yake ya usalama ya wilaya ikianzisha mchakato wa operesheni kwenye vyanzo vya maji kwa kuweka alama, kuvilinda na kupanda miti.

Habari Zifananazo

Back to top button