Chongolo aonya ucheleweshaji miradi ya Samia ya umwagiliaji 

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo ameziagiza Wizara ya Fedha na Mipango na ile ya Kilimo kukaa mguu sawa na kuhakikisha miradi ya Rais Samia Suluhu Hassan ya skimu za umwagiliaji haikwami kwa kutoa fedha kwa wakandarasi kwa wakati.

Chongolo ametoa maagizo hayo jana wilayani Chamwino baada ya kutembelea shamba la zabibu la Chinangali ikiwa ni siku ya nne ya ziara yake.

Alizitaka wizara hizo mbili kukutana na kuhakikisha fedha zinapatikana na kuwalipa wakandarasi wanaotekeleza miradi ya skimu za umwagiliaji ili kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi hiyo.

“Dhamira ya Rais Samia kwenye miradi ya umwagiliaji ni kuona tija inapatikana kwa haraka, sasa nendeni mkakae na mje na majibu ndani ya muda mfupi,” alisema na kuongeza:

“Hakikisheni mnaangalia ni namna gani mnakwenda kuongeza kasi ya utekeleaji wa miradi hii ambayo ina dhamira ya kujenga ukakika wa kilimo cha umwagiliaji kwa wananchi ili malengo ya Rais na serikali anayoiongoza yafikiwe kwa muda uliokusudiwa kwa wakati.”

Chongolo alikielekeza Chama cha Ushirika cha Wakulima wa zao la Zabibu kuanzisha mfuko maalumu ambao utatumika katika matengenezo ya mundombinu ya kilimo katika shamba hilo.

Pia alisema ni vyema kufikiria zaidi ya kuuza zabibu nje na kuja na mikakati wa kuhakikisha bidhaa za zao la zabibu zinatengenezwa ndani ya nchi na kuuzwa nje.

Katika hatua nyingine, Chongolo ameiagiza Ofisi ya Rais-Tamisemi kuja na mpango wa kutenga fedha kwa ajili ya kuhakikisha upatikanaji wa maji katika maeneo ya huduma za kijamii zikiwemo shule zote nchini.

Awali, Naibu Waziri wa Kilimo, Anthony Mavunde ameainisha mikakati katika kuhakikisha soko la zabibu linakuwa la uhakika ndani na nje ya nchi ikiwa ni pamoja na kuanzisha kiwanda cha kuchakata zabibu ili kuwa na uhakika kwa kuhifadhi mchuzi wa zabibu kwa muda mrefu.

Alisema pia serikali imeweka mkakati wa kuongeza kodi kwenye mvinyo kutoka nje ya nchi ili kuimarisha soko la ndani na kuendelea kuhamasisha wawekezaji ili katika ujenzi matanki makubwa ya kuhifadhi mchuzi wa zabibu.

“Pia tumepata mwekezaji mkubwa ambaye atakuwa anatengeneza juisi ambaye atanunua zabibu kwa wingi na pia tuko kwenye mazungumzo na TBL (Kampuni ya Bia Tanzania) waweze kuhifadhi mchuzi wa zabibu kwa muda mrefu,” alisema.

Kwa niaba ya wakulima wa zabibu, Waziri Mkuu Mstaafu na Makamu wa kwanza wa Rais Mstaafu John Malecela ametaja siri ya mafanikio kwa wananchi wa Dodoma kuwa ni kujikita katika kilimo cha zabibu.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
TUI BLUE Bahari Zanzibar
TUI BLUE Bahari Zanzibar
1 month ago

Watoto Wenye Tabia ZIFUATAZO WAMESHINDA NA WAMEAMUA MSHINDE KILA MMOJA MILION 60
•            MWIZI
•            BASHA (MAPENZI YA JINSIA MOJA)
•            MSAGAJI (MAPENZI YA JINSIA MOJA)
•            KICHAA
•            JAMBAZI
•            MALAYA
•            MLEVI
•            MUUAJI
•            TAILA
•            TASA
•            WABAKAJI
•            MLAWITI
•            MVUTA SIGARA
•            MVUTA BAGI
•            MTUMIA MADAWA YA KULEVYA
•            MTEMBEA UCHI
·             KIKOJOZI

KAMA UNA HIZI TABIA AU MWEZAKO ANA HIZI TABIA TUMA UJUMBE /JINA KWENDA 5660 AU PIGA 0800751000 BURE

Kwanza Resort by SUNRISE
Kwanza Resort by SUNRISE
1 month ago

Watoto Wenye Tabia ZIFUATAZO WAMESHINDA NA WAMEAMUA MSHINDE KILA MMOJA MILION 60
•            MWIZI
•            BASHA (MAPENZI YA JINSIA MOJA)
•            MSAGAJI (MAPENZI YA JINSIA MOJA)
•            KICHAA
•            JAMBAZI
•            MALAYA
•            MLEVI
•            MUUAJI
•            TAILA
•            TASA
•            WABAKAJI
•            MLAWITI
•            MVUTA SIGARA
•            MVUTA BAGI
•            MTUMIA MADAWA YA KULEVYA
•            MTEMBEA UCHI
·             KIKOJOZI

KAMA UNA HIZI TABIA AU MWEZAKO ANA HIZI TABIA TUMA UJUMBE /JINA KWENDA 5660 AU PIGA 0800751000 BURE

Melia Zanzibar
Melia Zanzibar
1 month ago

Watoto Wenye Tabia ZIFUATAZO WAMESHINDA NA WAMEAMUA MSHINDE KILA MMOJA MILION 60
•            MWIZI
•            BASHA (MAPENZI YA JINSIA MOJA)
•            MSAGAJI (MAPENZI YA JINSIA MOJA)
•            KICHAA
•            JAMBAZI
•            MALAYA
•            MLEVI
•            MUUAJI
•            TAILA
•            TASA
•            WABAKAJI
•            MLAWITI
•            MVUTA SIGARA
•            MVUTA BAGI
•            MTUMIA MADAWA YA KULEVYA
•            MTEMBEA UCHI
·             KIKOJOZI

KAMA UNA HIZI TABIA AU MWEZAKO ANA HIZI TABIA TUMA UJUMBE /JINA KWENDA 5660 AU PIGA 0800751000 BURE

Back to top button
3
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x