Chongolo aonya vijana kuendekeza kamari

KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo, amewaonya vijana kuacha kubahatisha maisha kwa kuendekeza kucheza kamari siku mzima na badala yake wajifunze ujuzi mbalimbali, ili wajiajiri na kukuza uchumi wao.

Kauli hiyo ameitoa leo katika Kijiji cha Ngerengere mkoani Morogoro, akiendelea na ziara yake mkoani humo kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM na kukagua uhai wa chama na kuzungumza na wananchi.

Chongolo amesema vijana wanapaswa kufanya kazi za kuwaingizia kipato na kuwataka vijana wasome ufundi wapate ujuzi badala ya kukimbilia kucheza kamari siku mzima.

“Acheni kushinda siku nzima na vikaratasi mnabeti, maisha sio kubahatisha kwa betting, mnakuwa watumwa, tafuteni kwenye vyuo vya ufundi kama VETA¬† mpate maarifa mjiajiri, najua wengi hawatafurahishwa na hili, lakini huo ndio ukweli,”amesema Chongolo.

Habari Zifananazo

Back to top button