Chongolo ashauri wananchi kufunga mita za maji

WANANCHI wa Kijiji cha Msolwa B wilayani Kilombero, wameshauriwa kufunga mita za maji katika nyumba zao, ili kulipa maji kadri wanavyotumia na kuepusha malalamiko yao ya kutozwa bei moja hata kama hawakutumia huduma hiyo.

Ushauri huo umetolewa leo na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Daniel Chongolo aliposimama na kusikiliza kero za wananchi hao,akiwa katika ziara yake ya kukagua Ilani ya chama kwa kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo na uhai wa chama.

“Tunaomba ndugu Katibu Mkuu utusaidie tunatozwa bei ya maji moja,kila mwezi shilingi 5,000 wakati wenzetu wanatozwa shilingi 2,000 au chini ya hapo,”wamesema wananchi hao kwa nyakati tofauti.

Akizungumzia hilo Chongolo alimtaka Kaimu Meneja wa Wakala wa Maji Vijijini (Ruwasa) Mkoa wa Morogoro, Sospeter Lutonja azungumzie, ambapo alisema tatizo lililopo eneo hilo ni wananchi kukataa kufungiwa mita za maji.

“Hawa wananchi walikataa kufungiwa mita za maji ambazo bili ya maji ingekuja kwa kadri ya kiwango cha maji ulichotumia, lakini kwa vile walikataa utaratibu ni kwamba wanalipa flat rate (bei moja) ambayo kwa mwezi ni shilingi 5,000,”amesema Lutonja.

Baada ya majibu hayo Chongolo amewashauri wafunge mita kwa wale wanaotaka ili kulipa bei ya maji kadri ya matumizi yao ,lakini kama hawataki waendelee na utaratibu uliopo wa kulipa kwa mwezi kwa bei elekezi.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x