Chongolo ataka majina wasiolipwa fidia

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Kondoa kumpa orodha ya wananchi ambao wamevamiwa na wanyama wakali na waharibifu na mpaka sasa hawajalipwa fidia.

Akiwa katika siku yake ya tano ya ziara katika majimbo ya Mkoa wa Dodoma, Chongolo ametaka orodha hiyo aipate kabla ya kumaliza ziara yake mkoani Dodoma.

Kauli ya Chongolo ameitoa kutokana na wananchi kubainisha uwepo wa changamoto ya uharibifu wa mazao yao kutokana na tembo na kutaka nguvu inayotumika kuwalipisha fidia wananchi pindi wanapokuwa wameingiza mifugo hifadhini, ndio itumike kulipa fidia wanapoathiriwa na tembo.

“Nataka nipewe orodha ya watu wote ambao wameathiriwa na wanyama wakali na wahalibifu kabla sijamalizia ziara yangu, halafu nimjue huyo anayekwamisha watu kulipwa fidia.”

Chongolo aliwashangaa watendaji ambao wanashindwa kuwajibika kufanya tathimin ya uharibifu unapotokea na kuwa kitendo hicho ni kuwachonganisha wananchi na serikali yao na kuchonganisha wananchi na CCM.

Chongolo aliwataka watendaji kuhakikisha wanafanya tathimini halisi na kwa wakati, ili wananchi waweze kufidiwa kutokana na madhara waliyoyapata.

Habari Zifananazo

Back to top button