Chongolo atoa ahadi Bwawa la Maji Kondoa

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Daniel Chongolo amewaahidi wananchi wa Kata ya Itaswi iliyopo Halmashauri ya Kondoa Vijijini kuwabana Waziri wa Fedha na Mipango na Waziri wa Maji kuhusiana na kuchelewa kuanza kutekeleza mradi wa bwawa la maji unaogharimu Sh bilioni 5.7.

Ahadi hiyo ameitoa baada ya Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dk Ashatu Kijaji kusema kingo za bwawa hili lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita za ujazo milioni 14 kupasuka hivyo kuchangia changamoto ya maji kwa Kata ya Itaswi na kata zinazozunguka kata hiyo.

” Tathimin imefanyika na tumefuata taratibu zote, lakini fedha zimekwishawasilishwa, lakini mpaka sasa mradi ambao ulipangwa kutekelezwa katika mwaka wa fedha 2022/23 haujaanza, tunaomba utusaidie kwa hilo,” amesema.

Chongolo amesema atakutana na mawaziri hao na kuwahakikishia wananchi kuwa ifikapo Julai 10 mwaka huu mkandarasi atanza kazi, ili kurejesha huduma ya maji kwa wananchi hao.

“Niwahakikishie kuwa ifikapo Julai 19 mwaka huu mkandarasi atakuwa site na kuanza kazi, kwa sababu mkandarasi anapopewa kazi ujue kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia kuwa fedha zitoke, na hii ndio Serikali inavyojali wananchi wake.”

Awali mtaalamu wa RUWASA alisema mchakato wote wa kutekeleza mradi huo imefanyika na kuuwasilisha Wizara ya Fedha na Mipango, tangu Novemba mwaka jana na mpaka sasa hakuna fedha zozote zimetolewa.

Aidha Dk Kijaji amemuomba Katibu Mkuu wa chama kumsaidia kumuombea chakula kutokana na wananchi wake kukabiliwa na njaa, baada ya kupata mvua chini ya kiwango na bwawa waliokuwa wakilitegemea kwa kilimo kuharibiwa na mvua zilizomuonesha mwaka 2021.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button