Chongolo atoa maelekezo ujenzi vituo vya afya

SERIKALI imeagizwa kuhakikisha kila kituo cha afya kinachojengwa nchini kwa sasa lazima kiwe na jengo la mama na mtoto pamoja na chumba cha upasuaji, ili kukabiliana na changamoto yoyote ya kiafya kwa kundi hilo.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amesema hayo leo baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha afya cha Haydom, wilayani Hanang mkoani Manyara.

Chongolo amesema lengo la kujenga majengo hayo ni kuhakikisha wanaondoa vifo vya mama na mtoto kwa asilimia 100 nchini.

“Ndio maana kila kituo cha afya kinachojengwa sasa lazima kiwe na jengo la mama na mtoto na jengo la upasuaji,ili changamoto zote za uzazi ziweze kushughulikiwa hapo hapo na kuokoa maisha ya mama na mtoto,”amesema Chongolo.

Amesema hilo linatekelezwa na ndio sababu serikali imeelekeza fedha nyingi kwenye ujenzi wa vituo hivyo, ili kulinda afya ya mama na mtoto na afya za wananchi wote kwa ujumla.

 

Habari Zifananazo

Back to top button