Chongolo: Kuuza ardhi ni kujitia umasikini

Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Daniel Chongolo ametoa wito kwa wananchi wa Bahi na wanaozunguka miundombinu ya umwagiliaji kutouza maeneo yao.

Chongolo ametoa rai hiyo wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Bahi.

“Pale serikali inapoboresha fedha za kuboresha miundombinu ya skimu za umwagiliaji wajanja wanaotafuta fursa wengi watakimbilia hapa kutafuta maeneo, acheni kuuza maeneo ya mashamba yenu.

Advertisement

“Yamilikini endeleeni kuyasimamia mtu akitaka kulima mkodishe alime akupe chako mwaka unaofuata ulime mwenyewe. Kuuza ardhi ni kujitia umasikini,” amesema.

2 comments

Comments are closed.