Chongolo RC Songwe

RAIS Samia Suluhu Hassan amemteua Daniel Chongolo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe.

Taarifa hiyo imetolewa leo Machi 9, 2024 na Ofisi ya Rais Ikulu katika taarifa ya mabadiliko madogo ya wakuu wa mikoa, wilaya, makatibu tawala na wakurugenzi.

Chongolo aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo miezi kadhaa iliyopita alijiuzulu nafasi hiyo.

Taarifa hiyo pia imeeleza kuwa Rais Samia amemteua Patric Kenan Sawala kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Sawala alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba.

Aidha, Paul Matiko Chacha ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, awali alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Misungwi.

Habari Zifananazo

Back to top button