Chuchu Hans azindua tamthilia yake

MWIGIZAJI Chuchu Hans kwa mara nyingine amezindua tamthilia ya Jeraha itakayorushwa kupitia chaneli ya sinema zetu.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa tamthilia hiyo jijini Dar es Salaam, Chuchu amesema haikuwa kazi rahisi lakini naamini Jeraha ni tamtilia itakayoleta mabadiliko makubwa na kuelimisha jamii ya watanzania wengi.

“Ni tamthilia iliyowakutanisha wakongwe wa Sanaa na wasanii chipukizi ambao wamefanya vizuri na kuonyesha uwezo wao vyakutosha” amesema Chuchu

Advertisement

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tamthilia hiyo Mkuu wa Idara ya Vipindi Fatma Mohamed, amesema kuwa jeraha ni tamthilia inayogusa maisha ya jamii husika.

“Tamthilia ya jeraha inagusa Mapenzi, visa na mkasa vilivyopo kwenye jamii yetu kuwaelimisha, kuwaburudisha na kuhasa jamii kwenye mambo mbalimbali.”

Pia ameongeza kuwa Sinema zetu tunalengo la kusaidia tamthilia zetu kufika nafasi za kimataifa zaidi na acha kubaki hapa hapa nchini.