Chukwuemeka nje wiki sita

MSHAMBULIAJI Carney Chukwuemeka wa Chelsea, atakuwa nje ya uwanja kwa wiki sita, baada ya kupata majeraha katika mchezo dhidi ya West Ham United Jumapili.

Dakika ya 28 ya mchezo huo, Chukwuemeka aliisawazishia Chelsea na mchezo kuwa 1-1, dakika ya 46 alitolewa baada ya kuumia na kuingia Mykhailo Mudryk hata hivyo mchezo uliisha kwa Chelsea kupoteza mabao 3-1uwanja wa London.

Taarifa ya Chelsea imeeleza Mwingereza huyo atafanyiwa upasuaji wa goti.

Advertisement

Chukwuemeka anaungana na Reece James, Wesley Fofana, Christopher Nkunku, Benoit Badiashile na Armando Broja ambao wote ni majeruhi.

Tembelea //epaper.tsn.go.tz kusoma zaidi.

una maoni usisite kutuandikia

6 comments

Comments are closed.