Chuo cha DMI kuja kivingine
ITALIA: CHUO cha Bahari Dar es Salaam (DMI) kimesaini Hati ya Makubaliano (MoU) ya kubadilishana uzoefu katika mafunzo ya ubaharia na kushirikiana katika tafiti na miradi ya maendeleo ya uchumi wa buluu na Chuo cha Italian Shipping Academy kilichopo nchini Italia.
MOU hiyo imesainiwa nchini Italia na Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam, Dk Tumaini Gurumo na Rais wa Chuo cha Italian Shipping Academy (FAIMM), Eugenio Massolo.
“Nimefurahi sana kuingia Makubaliano haya kwakua wenzetu wapo tayari kushirikiana nasi katika miradi mbalimbali, ninaona ndoto ya kufikia viwango vinavyokubalika na EU inakwenda kutimia,” amesema Dk Tumaini.
Makubaliano hayo yameshuhudiwa na Balozi Tanzania nchini Italia, Mahmoud Thabit Kombo na Balozi wa Italia nchini, Marco Lombardi.
Kwa upande wake Balozi Kombo amesema kuwa Italia imepiga hatua katika teknolojia hivyo utayari wao wa kushirikiana na DMI utaiwezesha zaidi Tanzania kukua katika eneo hilo. Vilevile Balozi Kombo ametoa wito kwa upande zote mbili kuteleza vipengele vya makubaliano ipasavyo ili izae matunda yanayotarajiwa.
Naye Mkuu wa Chuo cha FAIMM, Eugenio Massolo amesema kuwa makubaliano hayo yatasidia kukuza ujuzi kwa pande zote mbili ili kuendana na mahitaji ya soko la ajira.