WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso, ameitaka bodi mpya ya ushauri ya chuo cha maji kuja na mikakati ya kukikuza chuo hicho katika nyanja mbalimbali ili kukitofautisha na vyuo vingine.
Pia, Aweso, amekitaka chuo hicho kutumia fursa mbalimbali zilizopo hapa nchini kwa kuhakikisha wanaanzisha vyanzo vya mapato .
Aweso, ametoa maagizo hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya ya tano ya ushauri wa chuo cha maji.
“Rais Samia Suluhu pamoja na Wizara ya Maji wanaimani kubwa ya chuo cha maji kwa kuzalisha wataalamu ambao wanakwenda kushirikiana na serikali katika kutatua changamoto za upatikanaji wa maji.” Amesema
Hata hivyo, Aweso, amekitaka chuo hicho kuandaa mafunzo ya kipindi kifupi kwa mafundi bomba wa mtaani ili waweze kupata ujuzi ambao utawarahishia kwenye kazi zao.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa bodi iliyomaliza muda wake,Dkt Sara Khamis,amesema kwa kipindi kifupi walichokuwepo wameweza kuongeza udahili toka 1800 mpaka kufikia 2320 na kufanikisha kuongeza mitaala ya kufundishia.
Naye Mwenyekiti mpya ya bodi hiyo, Dkt Rehema Nchimbi, ameomba ushirikiano kwa manajement ya chuo hicho katika utendaji wa chuo hicho.