Chuo cha Mwalimu Nyerere wasaidia yatima

Wanafunzi na uongozi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere  jijini Dar es Salaam, wametoa mahitaji mbalimbali kwa watoto yenye thamani ya Sh milioni tano, wakati walipotembelea kituo cha watoto waishio mazingira magumu kiitwacho Orphanage Center, Kisarawe mkoani Pwani.

Lengo la mahitaji hayo ni kuwapa faraja na matumaini watoto waishio mazingira magumu, ambapo ni utaratibu wa chuo hicho kutoa msaada kwa wenye mahitaji maalumu kila mwaka.

Rais wa chuo hicho, Mohammed Hamad amesema  wakichokifanya kutoa msaada huo ni tendo la huruma kama dini zinavyohamasisha na kuwasihi wadau wengine nao kufanya hivyo.

Naye dada mlezi wa kituo hicho, Caroline Frank  amesema kituo hicho kinakabiliwa na changamoto nyingi, ikiwemo vitanda, ukuta wa kutengeneza,kuni,vyoo, na mahitaji mbalimbali.

Kwa upande wake Rais wa Orphanage Center, Baraka Matonge  amesema msaada huo utawasaidia kwa kiasi kikubwa na umewapa faraja, hivyo watu wasisite kuwatembelea.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button