City, Kovacic hakuna matata
KIUNGO wa Chelsea, Matteo Kovacic amefikia makubaliano binafsi ya kujiunga na Manchester City, baada ya mazungumzo ya kina wiki iliyopita.
Taarifa ya mwandishi wa habari za michezo, Fabrizio Romano imeeleza kuwa Kovacic anataka kuondoka klabuni hapo, hivyo mazungumzo yanayofuata ni Chelsea na Man City.
Amesema mazungumzo hayo yataanza baada ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itakayopigwa kesho mjini Istanbul, Uturuki.
Romano amesema Chelsea iko tayari kumuuza.