City, Liverpool kazi ipo leo

LIGI Kuu nchini England inarejea leo, baada ya mapumziko ya wiki mbili kupisha michezo ya kimataifa kufuzu mashindano ya Ulaya ‘Euro’ ambapo mchezo wa kwanza utakuwa kati ya Manchester City dhidi ya Liverpool, mchezo utakaopigwa Uwanjwa wa Etihad saa 8:30 mchana.

Mchezo wa kwanza uliopigwa Anfield Oktoba 16,202 Liverpool ilishinda bao moja lililofungwa na Mohammed Salah dakika ya 76.

Hata hivyo mchezo wa leo utatoa taswira kwa timu zote mbili kwa Liverpool kumaliza nafasi nne za juu au kwa Man City kupunguza gepu la pointi 9 dhidi ya vinara Arsenal wenye pointi 69.

Michezo mingine itakuwa kati ya Arsenal watakuwa Emirates dhidi ya Leeds United, Bournmouth dhidi ya Fulham, Crystal Palace dhidi ya Leicester City, Notts dhidi ya Wolver, Brighton na Brentford, michezo yote itapigwa saa 11:00 jioni.

Mchezo wa mwisho kwa leo utakuwa ni Chelsea dhidi ya Aston Villa utapigwa saa 1:30 usiku Uwanja wa Stanford Bridge.

Habari Zifananazo

Back to top button