City, United kuchapana mchana huu

LEO Manchester United watakuwa wenyeji wa Manchester City katika mechi ya Ligi Kuu England itakayopigwa saa 9:30 mchana katika Uwanja wa Old Trafford.

United wanaingia uwanjani wakiwa wameshinda mechi nane mfululizo na wanaweza kufikia historia ndefu zaidi ya kushinda katika michuano yote tangu Alex Ferguson alipostaafu kama meneja mwaka 2013.

City inayoshika nafasi ya pili, ambayo iko pointi nne juu ya United, ilifungwa na Southampton kwenye Kombe la Carabao Jumatano na kufanya kupoteza michezo mitatu msimu huu katika mashindano yote.

Advertisement

“Uboreshaji wa timu ya United uko wazi umeimarika,” alisema bosi wa City Pep Guardiola.
United itamkosa Anthony Martial mwenye jeraha la mguu hivyo Marcus Rashford ambaye amefunga mabao saba katika mechi sita zilizopita anaweza kucheza kama mshambuliaji wa kati.

Mchezaji mwingine atakayekosekana kwa upande wa United ni beki mreno, Diogo Dalot, kwa upande City itamkosa John Stones.

Michezo mingine ya EPL itakayopigwa leo ni Brighton dhidi ya Liverpool, Everton na Soton, Forrest na Leicester, Wolves na West Ham, mchezo wa mwisho ni Brentford na Bournemouth

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *