City, United mechi dume
MANCHESTER City itakuwa na kibarua kigumu watakapowakabili majirani zao Manchester United katika mchezo wa EPL utakaopigwa leo uwanja wa Etihad saa 12:30 jioni.
City, ambao walishinda 3-0 kwenye uwanja wa Old Trafford mwezi Oktoba, wanashika nafasi ya pili kwenye ligi, wakiwa nafasi nne juu ya United.
City hawajafungwa katika mechi 18 na United wamepoteza mara mechi moja mwaka huu.
“Ninachojifunza kutokana na uzoefu wangu katika aina hizi za michezo ni kuwa mtulivu zaidi, kupumzika, kutozungumza mambo mengi zingatia tu mbinu na kile unachopaswa kufanya ili kuzishinda, sio juu ya hisia,” amesema Guardiola.
Ushindi wa 1-0 wa Liverpool dhidi ya Nottingham Forest Jumamosi uliwasogeza kwa pointi nne City, ambao watasafiri hadi Anfield Machi 10 kuwavaa Liverpool.
Winga wa City, Jack Grealish hatokuwa sehemu ya mchezo huo baada ya kuumia paja katika ushindi wa Jumanne wa Kombe la FA raundi ya tano dhidi ya Luton.
Beki Josko Gvardiol anakaribia kurejea kutokana na tatizo la kifundo cha mguu lakini mchezo huu hatohusika.
Kiungo wa kati wa United Bruno Fernandes na mlinzi Raphael Varane walikuwa sehemu ya ushindi wa kombe la FA Jumatano huko Nottingham Forest licha ya matatizo ya kimwili na wanatarajiwa kuwepo.