CMSA watoa mafunzo uwekezaji Mwanza

MAMLAKA ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA)  kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya fedha  imetoa mafunzo ya kutambua fursa za uwekezaji  kwa vijana 100 kutoka mkoa wa Mwanza.

Akizungumza leo wakati wa mafunzo hayo Meneja wa uhusiano na elimu kwa umma kutoka mamlaka hiyo, Charles Shirima amesema kuwa kupitia jukwaa hilo  lengo ni kuwafundisha vijana namna ya kupata mitaji na kufanya biashara katika misingi bora na waweze kukua katika sekta hiyo.

Amesema jukwaa linatumia mfumo  wa Tehama ili kurahisisha kutoa miongozo ya kupata mafunzo hayo na pia itawasaidia kuanzisha majukwaa katika biashara watakazoenda kuzianzisha.

“Malengo yao yatafikiwa kwasababu hii ni njia nyingine labda kama wameshindwa kupata mtaji kwasababu hawakopesheki siku tukiweka jukwaa lingine kama hili litaweka njia nyingine ya kupata mitaji na lengo litafikiwa kwahiyo tunaamini wakifuata masharti lengo litaweza kufikiwa na watapata fursa kutoka kutoka Kwa Umma” amesema Shirima.

Kwa upande wake ofisa mipango na fedha kutoka Shirika la SIDO Mkoa wa Mwanza, Salum Msengi amesema vijana ambao wamehudhuria mafunzo hayo watakuwa mfano kwa vijana wengine katika jamii Kwa kutunisha mifuko ya hisa kupitia wao kwa wao Ili waweze kupata fedha ambazo hazitowaumiza na kuacha kwenda kukopa mitaani.

“Tunategemea waje wawe wajasiliamali wakubwa na kuzalishwa makampuni kwaajili ya kusafirisha bidhaa ndani na nje ya Nchi kwahiyo tunategemea kupitia vijana hawa  watanunua hisa na kutunisha mifuko”amesema.

Habari Zifananazo

4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button