COSOTA kutoa elimu kwa vyama na mashirikisho kutambua haki

MSIMAMIZI wa Haki Miliki (COSOTA)  Doreen Sinare amesema wameanza kutoa elimu kwa vyama na mashirikisho ya sanaa ili kuwajengea uwezo  wajue haki zao wakati wakitarajia kuunda makampuni ya kuwasimamia

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa utoaji wa Semina hiyo leo jijini Dar es Salaam, Doreen Sinare alisema kumekuwa na mabadiliko ya kimuundo katika yao hivyo kuna baadhi ya kazi zitafanywa kupitia makampuni yatakayoundwa na vyama na mashirika ya wasanii.

Alisema makampuni hayo yatakuwa yakisimamia kazi zote za wasanii ikiwemo kukusanya mirabaha na kazi zingine, hivyo kupitia kamati iliyoundwa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na michezo ikataka Ofisi hiyo kuwapa wanachama na mashirikisho ya wasanii.

Doreen alisema wameanza na Shirikisho la Sanaa za maonesho ambalo linaundwa na wasanii wa ubunifu wakiwemo MC, Wanamuziki, Washairi watunzi na wengine ambapo waliudhulia zaidi ya viongozi  30 kati ya wasanii viongozi  50 walioarikwa.

“Leo tunawajengea uwezo, na kuwapa moyo jinsi gani ya kuanzisha hayo  makampuni na jinsi ya kuyasimamia .

Upande mwingine kuwapatia elimu ya haki miliki, wao ni moja ya wadau ambao ni wabunifu katika eneo lao wanatakiwa kulindwa na kujua ni jinsi gani wanaweza kunufaika” alisema.

Mwenyekiti wa bodi Sanaa za maonesho Tanzania, Betty Kazimbaya aliipongeza COSOTA na kusema semina hiyo inawasaidia kufahamu nini maana ya haki miliki na faida ambayo msanii ataipata baada ya kujisajili.

Anasema imekuwa kawaida kwa wasanii wengi kutokwenda kusajili kazi zao , kutokana na kutokuwa na uelewa hivyo wanazurumiwa  au kuzurumu wengine bila kujua.

Habari Zifananazo

Back to top button