Dabo kocha mpya Azam FC

Dabo

KLABU ya Azam FC imemtangaza Youssouph Dabo kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo kwa msimu wa ujao wa 2023/24.

Akizungumza wakati wa utambulisho huo, Mtendaji Mkuu wa timu hiyo Abdulkarim Amin ‘Popat’, amesema kilichowavutia kwa kocha huyo ni mafanikio aliyoyapata hasa kwenye michuano ya kimataifa akiwa na timu ya Teungueth FC ya Senegal.

“Nikocha bora ambaye naamini atabadilisha mwenendo wa timu yetu katika muda huo wa miaka mitatu tutakayokuwa naye hapa Azam hasa kwenye michuano ya kimataifa, ambayo ndio lengo letu kubwa msimu ujao,” amesema Popat.

Advertisement

“Karibu sana Azam FC Youssouph Dabo,” amesema Popat na kueleza kuwa kocha huyo amesaini mkataba wa miaka mitatu.