DAKTARI wa magonjwa ya binadamu, Grace Mapunda amesema aliandika kitabu cha Sonona Kazini baada ya watu kufikiri madaktari hawaathiriki na magonjwa ya akili.
Akizungumza na mwandishi wa gazeti la Habari Leo, Grace Mapunda alisema watu wengi wamekuwa wakiamini daktari ni mtu ambaye anajua vitu vingi hasa vinavyohusiana na afya.
Alisema Jambo hilo sio kweli, hata yeye limemkuta ingawa ni daktari lakini aliweza kukubwa na ugonjwa wa afya ya akili uliopiliza hadi kufikia hali ya Sonona.
Grace alisema ugonjwa huo aliupata baada ya kufiwa na mzazi wake, hivyo alijikuta katika hali mbaya ya mawazo kiasi cha kupatwa na ugonjwa huo ambao kwa sasa umekuwa tishio duniani.
“Kupitia changamoto ambazo Mimi nimepitia, nikaona niandike kitabu ili kuwafundisha watu kwamba haya magonjwa ya akili ikiwemo Sonona wanaweza kuugua yoyote” alisema.
Alisema kupitia kitabu hicho ambacho ni kidogo, mtu anaweza kukibeba popote, amejaribu kufafanua namna ya ugonjwa huo unavyoanza na jinsi unavyoathiri watu wengi.
Aliongezea kwa kusema lakini pia aliandika sehemu kidogo ya maisha yake, ili watu wajifunze kupitia yeye na waone kwamba ugonjwa huo anaweza kuugua yoyote.
“Ni kitabu ambacho najaribu kuwaambia watu wanapoona dalili hizi au zile kwamba nini wafanye ili kunusuru maisha yao” alisema.Alisema athari Kubwa ya ugonjwa huo kwamba mtu wanaweza kujidhuri mwenyewe au anaweza kumdhuri mtu mwingine.
Grace alisema kwa sasa amechaguliwa kuwa katika Kamati ya Afya Malezi na Afya chini ya Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es salaam na Mjumbe wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania.
Comments are closed.