Daktari aeleza madhara ya kunywa maji kupita kiasi

DAKTARI Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Samuel Rweyemamu amesema unywaji maji kupita kiasi si tiba ya moyo bali ni chanzo cha matatizo zaidi mwilini.

Dk Rweyemamu amelazimika kusema hayo leo Alhamisi jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya Siku ya Moyo Duniani baada ya dhana ya kunywa maji mengi kusambaa mitandaoni.

Ila ifikapo Septemba 29 dunia huadhimisha Siku ya Moyo.

“Kuna mtu aliniambia anakunywa lita tano kwa siku sasa nasikitika sana tunapokuona umevimba maji yamejaa mwilini sasa tunakupa dawa ukojoe..kuna mwingine mkojo uliisha siku mbili.

“Mmoja akauliza huu mkojo ulikuwa unakaa wapi? lakini kumbe mwili umejaa maji yakaisha mapafu yakawa vizuri na akatembea vizuri,” alieleza.

Akitoa ushauri juu kiasi kinachotakiwa, mtaalam huyo alisema, mtu mwenye tatizo la moyo anatakiwa kunywa maji lita moja na nusu tu kwa siku moja.

“Kinyume chake watu wanakunywa maji wakidai yanatibu moyo huu ni uposhaji wa kwenye mitandao.

Kunywa maji kawaida mtu mwenye shida ya moyo anywe maji lita moja na nusu na sio maji tu vimiminika vyote, supu kidogo, maji isizidi lita moja na nusu,”amesisitiza Dk Rweyemamu.

Amasema takwimu zilizopo watu zinaonesha kuwa takribani milioni 17 wanaweza kuwa na matatizo ya moyo .

Habari Zifananazo

Back to top button