Daktari feki ‘Ustadhi’ akamatwa Muhimbili

MKAZI wa Dar es Salaam aliyejitambulisha jina la Mussa Mawa amekamatwa katika maeneo ya Hospitali ya Taifa Muhimbili akijihusisha kutapeli wananchi wanaopata huduma kwa kujifanya daktari.

Daktari huyo feki ambaye amedai kazi yake ni Ustadhi, ametokea maeneo ya Mbagala jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Idara ya Ulinzi Alfred Mwaluko amesema kuwa wana usalama walimbaini daktari huyo feki akiwa kwenye harakati za kuwatapeli wananchi wanaouguza ndugu zao waliyelazwa jengo la Mwaisela.

Akizungumza leo Agosti 30, 2023  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma, Aminiel Aligaesha amesema daktari huyo feki alikuwa kwenye harakati za kumuibia mgonjwa sh 140, 000.

 

Pia alipohojiwa kuhusu koti la udaktari alikolitoa pamoja na kitambulisho, daktari huyo feki anasema alianua koti hilo likiwa limeanikwa huku akidai kuwa kitambulisho kakipata maeneo ya hospitali hiyo kuna mtu alikuwa anatengenezesha.

Kufuatia hali hiyo, Aligaesha amewataka watu wote wanaojihusisha na kutapeli wananchi katika eneo la Hospitali hiyo kwamba kwa sasa ulinzi umeimarishwa na wakijaribu kufanya hivyo watakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya usalama.

Habari Zifananazo

5 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button