Daktari wa Tanzania afariki Uganda kwa Ebola

DAKTARI Mtanzania aliyekuwa akisoma nchini Uganda amefariki dunia baada ya kuambukizwa virusi vya Ebola. Anakuwa daktari wa kwanza kufariki kutokana na ugonjwa huo.

-Waziri wa Afya wa Uganda Jane Ruth Ocero alitoa tangazo hilo Jumamosi kwenye ukurasa wake wa Twitter.

“Nasikitika kutangaza kuwa tumempoteza daktari wetu wa kwanza, Dk Mohammed Ali, Raia wa Tanzania, mwanaume mwenye umri wa miaka 37 leo saa 3:15 asubuhi,” aliandika.

Ocero amesema daktari huyo alifariki alipokuwa akipokea matibabu.

“Alipimwa na kuambukizwa Ebola mnamo Septemba 26, 2022, na alikufa alipokuwa akipokea matibabu katika Fort Portal RRH, kituo cha Kutengwa (JMedic).”

 

Ocero akiwapa pole familia ya marehemu.

“Natoa pole kwa familia yake, madaktari, chuo kikuu cha KIU na wananchi wa Tanzania. Dk Ali ni daktari wa kwanza na mhudumu wa afya wa pili kufariki kwa ugonjwa wa Ebola. Wa kwanza alikuwa mkunga kutoka kliniki ya St Florence. alikufa kabla ya kupimwa,” alitweet.

Idadi ya watu wanaoshukiwa kuwa na Ebola inaendelea kuongezeka nchini Uganda.

Ebola ni ugonjwa mbaya na ambao mara nyingi huwa mbaya sana unaosababishwa na virusi vya Ebola.

 

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x