Daladala, bajaji marufuku kuweka sime, panga

MKUU wa Mkoa wa Arusha, John Mongella amepiga marufuku kwa vyombo vya usafiri daladala na bajaji kuwa na silaha kama sime au mapanga na endapo vyombo hivyo vikikutwa na silaha hizo vitafutiwa leseni za usafirishaji.

Mongella ametoa agizo hilo leo jijini Arusha wakati akizungumza na madereva wa daladala na wamiliki wa vyombo hivyo kwa ajili ya kupata suluhu na kuongeza kuwa kesho atakutana na madereva wa bajaji, kisha Ijumaa watakaa kwa pamoja kupata suluhu ya changamoto zao.

Advertisement

Alihoji kwa nini silaha ziwepo katika magari na kama ikitokea kutoelewana na silaha inaonekana inaweza kusababisha matatizo, hivyo kuonya kwamba kusitokee upande wowote kuupiga mwingine kwani hatua zitachukuliwa.

“Daladala wan ahoja zao na bajaji wana hoja zao, lazima niwasilikize nijue wapi pa kuanzia, angalieni mgomo wa juzi watu wazima wanapanda Kirikuu na wanafunzi wanatembea inasikitisha, ofisi yangu haina mipaka unajua mimi ni baba siwezi kutembea na viboko kila mahali, lakini nawaambia suala la migomo halileti afya hapa Arusha,” amesema.

2 comments

Comments are closed.