Dalali, Rage, Aveva, Swed wapewa jukumu Simba

DAR ES SALAAM: RAIS wa heshima wa Klabu ya Simba ya Dar es Salaam, Mohamed Dewji amefanya uteuzi wa wajumbe wa bodi ya Baraza La Ushauri Simba Sports Club Company Limited.

Kupitia taarifa aliyochapisha katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram leo, Dewji ameandika:“Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita tangu tuanze safari ya mabadililko klabu yetu imepiga hatua kubwa sana katika nyanja mbali mbali. Pamoja na maendeleo ambayo Klabu yetu imepiga katika kipindi hiki cha miaka mitano lakini malengo yetu bado hatujayafikia.”

Amesema kama Rais wa heshima wa Simba jukumu lake ni kuhakikisha uongozi na utawala bora unazidi kuboreshwa kila wakati ili kuzidi kusukuma gurudumu la maendeleo ya klabu hiyo.

Advertisement

“Hivyo basi, baada ya kushauriana na Mwenyekiti wa Bodi na Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, nimewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Baraza la Ushauri ( Advisory Board) la Klabu ya Simba,” ameandika kiongozi huyo.

Amewataja aliowateua kuwa ni  Jaji Thomas Mihayo, ambaye atakuwa Mwenyekiti, ambapo wajumbe wengi wao wakiwa ni majina yaliyozoeleka katika uongozi wa mpira wa miguu ikiwa ni pamoja na kushika nafasi mbalimbali za uongozi maeneo tofauti ni Hassan Dalali, Ismail Aden Rage,  Evans Aveva na Faroukh Baghoza.

Wengine ni Swedi Nkwabi, Azim Dewji, Kassim Dewji, Musleh Al-Ruweh,Mohamed Nassor, Mulamu Ng’ambi,  Octavian Mshiu, Prof Janabi, Hassan Kipusi,  Geofrey Nyange, Gerald Yambi, Moses Kaluwa, Crescentius Magori, Juma Pinto- Mjumbe, Mwina Kaduguda na Idd Kajuna.

“Kazi kubwa ya Baraza hili itakuwa ni kuishauri Bodi juu ya maendeleo ya Klabu yetu ya Simba, uongozi na utawala bora,” amesema.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *