Dani Alves jela miaka minne

BEKI wa zamani wa Barcelona na Brazil, Dani Alves amehukumiwa kifungo cha miaka minne na miezi sita jela baada ya kukutwa na hatia ya kumnyanyasa kingono msichana mdogo akiwa kwenye moja ya kumbi za starehe huko Barcelona, mahakama nchini Hispania imeamua leo.

Pia mahakama imemtaka Alves kulipa Euro 150,000 kwa msichana huyo. Alves, mwenye umri wa miaka 40, alikana kosa hilo wakati wa kesi iliyoendeshwa kwa muda wa siku tatu mwezi huu hata hivyo uamuzi huo anaweza kukata rufaa.

Mahakama ilimkuta na hatia Alves na kwamba tukio hilo lilifanyika asubuhi ya Desemba 31, 2022, katika bafu la kumbi hiyo.

Beki huyo alikamatwa Januari 2023. Amezuiliwa tangu wakati huo na maombi ya dhamana yalikataliwa kwani mahakama iliona pengine angeweza kukimbia.

 

Habari Zifananazo

Back to top button