ILI kudhibiti nidhamu kwa wanafunzi wa shule za Sekondari, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema wapo kwenye mchakato wa kufuta shule zote za Sekondari za kutwa.
Chalamila ameyasema hayo leo Agosti 14, 2023 katika uwanja wa shule ya Sekondari ya Azania kwenye hafla ya kukabidhi magari kwa maafisa elimu wa sekondari kutoka wilaya nane.
Amesema, Mkoa wa Dar es Saalam una shule za sekondari 182 na za binafsi zipo nyingi zaidi ya 200.
“Katika Mkoa tunapokea sh billion 1.3 fedha zinazohudumia wanafunzi kama ada na posho ya madaraka kwa walimu.
Amesema, pamoja na kwamba Dar es Salaam ina shule nyingi, kidato cha sita ndio inafanya vizuri katika matokeo lakini kidato cha nne bado ni changamoto kwa sababu kuna shule nyingi sio za bweni.
” Na kwa sababu ya vitendo vingi vinavyoendelea mitaani ikiwemo ukosefu wa maadili, foleni sisi tumeshakaa kikao chetu na shule zetu, tumepanga mipango kwamba sasa tujipe muda tuanze kufuta shule za kutwa ili hapa katikati kote tuwe na shule za bweni tu..”, mesema Chalamila na kuongeza
“Tutafuta shule za kutwa tubaki na Bweni hii itasaidia kumanage nidhamu ya wanafunzi katika makuzi yao lakini pia muda wanaofika shule na hata walimu wa ziada ni rahisi kuweza kuwamanage wanapokuwa pamoja.
“Tutakuletea concept mezani mh Waziri ( Angela Kairuki – Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi) kwako ili kama kuna wafadhili basi wafikirie pia Mkoa wetu, si tu kuwa na shule nyingi ni kwamba una wanafunzi pia wengi.” Amesema
Aidha, Chalamila ameomba shule zote za Dar es Salaam kufungiwa umeme wa Sola kupitia miradi mbali mbali ya Tarura.
” Mh Waziri kwenye haya mashule badala ya kutumia umeme wa gridi ya taifa, program ya barabara za Tarura kuna ‘package’ ya taa, naomba angalau kupata taa 10 kwa kila shule zikafungwa ili kupunguza adha ya kulipa bili ya umeme kwa hizi shule na kuwapunguzia gharama
Comments are closed.