Dar kujinafasi riadha Mei 25

DAR ES SALAAM: Mashindano maalum ya riadha yanayojulikana kama ‘Run for Binti’ msimu wa tatu yanatarajia kufanyika Mei 25 mwaka huu katika Viwanja vya Oyesterbay jijini Dar es Salaam.

Dhamira ya mashindano hayo kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa LSF, Lulu Ng’wanakilala ni kuwezesha watoto wa kike kupata mazingira bora ya elimu pamoja na afya ya uzazi.

“Katika utekelezaji wa mradi wetu wa upatikanaji wa haki nchini tumeona dhahiri  kwamba wasichana wanakabiliana na vizuizi visivyozuilika na vinavyozuilika katika kupata elimu, huduma za afya, na haki zao za msingi.

Advertisement

“Kupitia mbio za mwaka jana tuliwezesha ukarabati na ujenzi wa miundombinu ya vyoo na usambazaji wa taulo za kike na utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti mashuleni na hivyo kuwawezesha wanafunzi zaidi ya 2500 katika shule za sekondari za Mtwara kunufaika.”amesema Lulu.