Dar kusambaziwa nishati ya gesi asilia

DODOMA; NAIBU Waziri wa Nishati Judith Kapinga amesema serikali ina mpango wa kusambaza nishati ya gesi asilia kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam 10,000, ili kuhakikisha kila Mtanzania anatumia gesi hiyo.

Akijibu swali mjini Dodoma, Naibu Waziiri Kapinga amesema kwa sasa serikali kusambaza nishati ya gesi asilia katika nyumba 880 katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Amesema malengo ya serikali ni kuhakikisha kila mtanzania hadi yule anayeishi vijijini aweze kutumia gesi hiyo kwa uhakika na kwamba mkakati uliopo kwa sasa kuendelea kuhamasisha jamii kutumia nishati ya gesi asilia.

Habari Zifananazo

Back to top button