Daraja jipya la Wami Ruvu kuanza kutumika Sept. 30

DARAJA Jipya la Wami lenye urefu wa mita 513.5 na barabara unganishi ya kilometa 3.

8 litaanza  kutumika Septemba 30, 2022.

Akizungumza katika ziara yake leo Septemba 18, 2022 Katibu, wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Shaka Hamdu Shaka amesema CCM imeridhishwa na ujenzi wa daraja hilo la Wami ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 89.

“Daraja hili lilianza ujenzi mwaka 2018, hadi Rais Samia Suluhu Hassan anaingia madarakani ujenzi ulikua umefika asilimia 47, lakini ndani ya mwaka mmoja wa Rais Samia, kasi imeongezeka kwa asilimia 42 na sasa wataalamu wanatuambia ujenzi umefikia asilimia 89,” amesema Shaka na kuongeza.

Katibu, wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Shaka Hamdu Shaka

“Pongezi zetu ziwafikie wakandarasi ndani ya kipindi kifupi tuliambiwa daraja hili lingeanza kazi Septemba 20 tukasema haitawezekana lianze kazi kabla ya chama kufika hili jambo ni kubwa, ni utekelezaji wa ilani ya CCM ibara 55  (d) (1)….; “CCM inaridhishwa, na kazi zinazofanywa na serikali” alisema.

Alisema daraja hilo limebeba maslahi mapana ya Watanzania kwa kuwa  linakwenda kuunganisha Mikoa yote ya Kaskazini na nchi jirani ikiwemo Kenya hivyo fursa ambazo zitatokana na daraja hilo ni nyingi hasa kiuchumi.

“Sekta ya usafiri na usafirishaji itahimarika kuliko ilivyo sasa kipindi cha nyuma madereva walikuwa wakikatisha ruti zao wakihofia usalama wa barabara hii usalama wa mali zao na usalama wa watu wao ambao wamekuwa wakiwatuma kazi,”Alisema Shaka.

Muonekano wa barabara ya maunganisho daraja la wami ruvu ambalo ujenzi wake bado unaendelea

Alisema athari iliyopatikana kutokana na ufinyu wa daraja la awali ni mkubwa kuliko wanavyofikiria na Rais Samia Suluhu Hassan alivyoingia madarakani kulikuwa na maneno mengi kuhusiana na daraja hilo na sio hilo tu na miradi ya mikakati kutokuendelea.

Shaka alisema, Rais Samia wakati anapokea kijiti daraja hilo kwa miaka mitatu lilijengwa kwa asilimia 47 leo hii ndani ya miezi 18 amesimamia ujenzi wa daraja hilo na kujengwa kwa asilimia 42.2.

Alisema fedha zote zimetoka kwa muda unaotakiwa na endapo isingetoka kwa wakati wakandarasi wasingeonyesha kazi kubwa iliyofanyika na kufikia asilimia 89.2.

“Kazi kubwa imefanyika ndani ya muda mfupi wa Rais Samia hapa unaona namna gani Watanzania wananufaika na kodi zao fedha zote zilizotoka katika mradi wa daraja hili ni fedha ya ndani sio fedha ya msaada ni ya walipa kodi ya Watanzania ndio iliyofanya hii kazi,”alisema Shaka.

Alisema wataalamu wamemueleza katika historia ya nchi hilo litakuwa ni daraja la kwanza kukamilika kabla ya wakati uliokadiriwa.

Alisema daraja hilo lilikadiriwa kutumia miaka minne litafunguliwa kabla ya Novemba wanakimbizana usiku na mchana kuhakikisha mwisho wa Septemba daraja linaanza kazi.

Ziara ya Shaka Wami Ruvu

Aidha, Shaka alisema kuna haja ya kumpongeza Rais Samia kwa maendeleo anayoyafanya ya nchi na wawe tayari kuyaeleza anayoyafanya kwa maslahi ya wananchi na Tanzania.

Alisema chini ya uongozi wa Rais Samia wataimarisha huduma zote za kijamii, kiuchumi na kisiasa ndani ya nchi.

Shaka alisema Rais Samia amedhamiria kufanya mambo makubwa na ifikapo mwaka 2025 hawatapata shida katika kufanya kampeni amesaidia kufungua fursa ndani ya nchi.

“Miradi ya maendeleo inaendelea, fursa za kiiuchumi zinakuja, mahusiano yetu yanafunguka. Rais Samia amekuwa na uongozi shirikishi,funganishi na viongozi karibu asilimia 90 walioteuliwa na Rais wanafanya kazi vizuri,”alisema Shaka.

Aidha, Shaka aliwaomba Wana CCM kuendelea kutoa ushirikiano kwa viongozi wa serikali na kwa Rais Samia ambae dhamira yake ni njema kwa Watanzania wale wachache ambao wanafikiria wao hawapo huko nia ni moja kuiongoza Tanzania na kuhakikisha ahadi wanazitekeleza.

“Mgombea wetu wa Urais yupo Samia Suluhu Hassan, kwa sasa tunakimbizana na maendeleo ya Watanzania hiyo ndio kazi tuliyonayo tusipoteze kujadili mgombea urais 2025 sisi hatuangaiki na mgombea wa Urais maana tunaye tunasubiri muda na kazi anayoifanya mnafikiri ni nani atamnyima kura,”alihoji Shaka.

Awali akizungumza Meneja wa Wakala wa Barabara (Tanroads), Mhandisi Baraka Mwimbage, alisema ujenzi wa daraja hilo ulianza mwaka 2018 na kwa sasa upo kwenye hatua za mwisho kukamilika ili kuukabidhi kwa serikali rasmi mwezi Novemba.

Alisema lengo la daraja jipya ni kutatua changamoto zitokanazo na daraja la zamani ambalo kwa sasa halikidhi mahitaji ya magari yanayopita kwa kuwa lilijengwa miaka 63 iliyopita ni jembamba lenye njia moja.

Mwimbage alisema daraja hilo litakapokamilika litagharimu shilingi bilioni 74 litakua na njia mbili za magari za mita 4, njia ya waenda kwa miguu pamoja na taa za mionzi ya jua zenye kamera 21 zikiwekwa umbali wa mita 25 kila upande

Naye Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, alisema anamshukurua Rais Samia kwa fedha walizopatiwa za miradi ya kimaendeleo itasaidia kuongeza fursa za kiuchumi.

Habari Zifananazo

Back to top button