Daraja la Chelsea kumvusha Martinez?

ENGLAND; Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina na Inter Milan ya Italia, Lautaro Martinez amekuwa shabaha kuu ya Chelsea katika dirisha la usajili la majira ya joto, ikiwa timu hiyo itamkosa Victor Osimhen.

Mtandao wa michezo wa HITC wa nchini Uingereza umeripoti kuwa chaguo la msingi la Chelsea kwa nafasi ya mshambuliaji ni Victor Osimhen wa Napoli, ambaye inaaminika bei yake imeshuka hadi pauni milioni 95 kutoka pauni milioni 150 majira ya joto yaliyopita.

Hata hivyo, ikiwa Chelsea itashindwa kumpata Osimhen, huenda wakaelekeza mawazo yao kwa Martinez.

Advertisement

Licha ya kuwa na miaka miwili kwenye mkataba wake, Inter ina matumaini ya kuongeza muda wa kusalia kwa Martinez na iko tayari kumfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi.