Darts yapewa tano ujio wa kadi maalum

NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Miundombinu, Mhandisi Rogatus Mativila amepongeza wakala wa mabasi yaendayo haraka (Dart) kwa kutumia mfumo wa kudhibiti kugushi tiketi (msimbo code) na kuanza mchakato wa matumizi ya kadi maalum kwa wateja wake.

Mhandisi Mativila ametoa kauli hiyo, jijini Dar es Salaam alipotembelea ofisi hiyo na mradi wa mabasi yaendayo kwa haraka awamu ya kwanza na ya pili katika eneo la Gerezani, pamoja na mpango mkakati wa Dart wa kuanzisha eneo la kibishara mkabala na kituo hicho cha Gerezani.

Naye, Mtendaji Mkuu wa Dart, Dkt. Edwin Mhede amesema Dart ina mpango wa kuanza rasmi matumizi ya kadi mapema baada ya mwezi Machi mwakani.

“Tayari kadi zimekwishanunuliwa na mchakato wa kufunga mfumo wa kadi unaendelea na Mwezi Machi utaanza kuwekwa kwenye mageti,”amesema.

Pia, amesema Dart inatarajia kuanza safari kutoka Mbagala hadi Gerezani mapema mwezi Machi, 2024.

Habari Zifananazo

Back to top button