DAS Same awapa somo wanafunzi Umiseta

KILIMANJARO: KATIBU Tawala wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, Upendo Wella amewataka wanafunzi wa wilaya hiyo watakoshiiriki mashindano ya UMISETA ngazi ya mkoa kutanguliza nidhamu.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Same, Kasilda Mgeni, Upendo Wella amewataka pia wanafunzi hao kuendelea kujikita kwenye masomo na sio vinginevyo.

Sambamba na hilo niwaombe pia wanafunzi ambao mnashiriki mashindano ya UMISETA, kuendelea kujikita zaidi kwenye masomo yenu ili kutimiza ndoto zenu kwenye maslahi mapana ya taifa letu,” amesema Upendo Wella.

Pia amewasisitizia walimu, wafanyakazi na wanafunzi kudumisha na kuendeleza michezo, kwakuwa ni afya, ajira na hudumisha mahusiano mazuri kwa vijana.

“Michezo inaleta maendeleo makubwa katika taifa letu. Ndiyo maana tunamuona Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, anavyotoa hamasa kubwa kwa timu zetu hapa nchini kwenye mashindano tofauti ndani na nje ya nchi,” ameongeza Upendo Wella.

Habari Zifananazo

Back to top button