Davido aikumbuka jamii yenye uhitaji

NIGERIA: Msanii kutoka nchini Nigeria David Adeleke maarufu ‘Davido’ na Taasisi yake wametangaza kutoa kiasi cha Naira milioni 300 ambayo ni sawa na Sh millioni 504.8 ili kusaidia vituo vya Watoto yatima nchini Nigeria.

Msanii huyo maaarufu Afrika na nchini kwao amesema ameamua kuimbuka jamii ya wenye uhitaji katika kufurahia mafanikio yake katika muziki hivyo ameona ni vyema kurudisha shukrani zake kwa vituo vya watoto yatima  vilivyopo nchini Nigeria.

Huu umekuwa ni utaratibu kwa wsanii mbalimbali kutoka taifa hilo la Magharibi mwa Afrika ambapo Mwaka 2023, OBO na DAF walichangia Naira milioni 237 ili kusaidia vituo vya watoto yatima nchini humo na sasa Davido naye ameamua kuikumbuka jamii hiyo.

Advertisement